ELCT Press Release

Date: August 9, 2017
Press release No. 001/08/2017

close window


Matengenezo: Tumeokolewa kwa Neema ya Mungu
(English)

August 9, 2017
Press release No. 001/08/2017

“Tumeokolewa kwa Neema ya Mungu” ni kauli mbiu iliyochaguliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kuongoza maadhimisho ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa 2017. Ifuatayo ni KKKT ratiba ya Juma la Matengenezo kuanzia ngazi ya sharika hadi kitaifa:

NGAZI YA DAYOSISI

Kamati inaafiki Azimio la kuwa na bustani ya miti lenye ua kama ilivyo nembo ya Dkt. Martin Luher na baada ya majadiliano ilipatana mambo haya ya ziada:

 • Pawepo bustani au shamba la miti kwa kumbukumbu hiyo Kidayosisi /au Sharikani
 • Maadhimisho yafanywe na Dayosisi, Sharika na Vituo vyote vya Kanisa
 • Kwaya zote zijiandae kwa wimbo wa halaiki
 • Kwaya zote zijiandae kwa tamasha la uimbaji
 • Juma la kumbukumbu ya miaka 500 ya matengenezo ni tangu 1 – 8 Octoba 2017

NGAZI YA SHARIKA NA VITUO

1 Oct Jumapili

 • Iwe ni Siku ya mwanzo ya juma la maadhimisho
 • Ibada maalumu ifanyike
 • Mtaalamu awepo kufundisha kusudi na historia ya Matengenezo ya Kanisa
 • Tamasha la Uimbaji

2 Oct Jumatatu

 • Iwe ni Siku ya Vijana
 • Miti ipandwe
 • Kujitolea damu inapowezekana
 • Watembelee watu walio na uhitaji katika jamii

3 Oct Jumanne

 • Iwe ni Siku ya Wanaume
 • Wanaume na Huduma za Udiakonia
 • Maombi kwa wagonjwa
 • Usafi wa mazingira
 • Kongamano la wanaume na wavulana

4 Oct Jumatano

 • Iwe ni Siku ya Wanawake
 • Wanawake na Huduma za Udiakonia
 • Maombi kwa wagonjwa
 • Usafi wa mazingira
 • Kongamano la wanawake na wasichana

5 Oct Alhamisi

 • Iwe ni Siku ya Vituo vya Kanisa ngazi zote
 • Vipindi vya dini mkazo uwe kuhusu matengenezo
 • Watoe huduma za kijamii
 • Wapate maelezo ya kusudi na historia ya matengenezo
 • Utoaji damu inapowezekana

6 Oct Ijumaa

 • Iwe ni Siku ya Watoto
 • Mchungaji aongoze Ibada ya Watoto
 • Igizo
 • Kwaya au nyimbo

7 Oct Jumamosi

 • Iwe ni Siku ya Watu wote
 • Usafi wa mazingira
 • Tamasha la uimbaji

8 Oct Jumapili

 • Iwe ni Siku ya Kilele
 • Ibada iwe ni moja tu inapowezekana
 • Kwaya ya halaiki iimbe siku hiyo
 • Tamasha la Uimbaji

NGAZI YA KITAIFA

 • Kanisa limeteua Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira (TUMA) kuwa eneo la kuadhimisha miaka 500 ya matengenezo kitaifa.
 • Kongamano la kitaifa litafanyika 7/10/2016 ambapo mada mbalimbali zitatolewa na kujadiliwa na wajumbe toka dayosisi 25 za KKKT.
 • Tarehe 8/10/2017 itafanyika ibada maalumu ya kilele cha miaka 500 ya matengenezo.

 


Reformation: Liberated by God’s grace
(Kiswahili)
             (close window)

August 9, 2017
Press release No. 001/08/2017

“Liberated by God’s grace” is the theme chosen by the Evangelical Lutheran Church in Tanzania (ELCT) for the 500th anniversary of the Reformation in 2017. The following is the programme to be carried out on both parish and national levels:

AT DIOCESE LEVEL

 • To set aside a tree planting to mark 500 years of reformation at diocese and parish level
 • Celebrations of the Reformation to be observed by dioceses, parishes, institutions and the church at the national level
 • All parishes to prepare for a mass choir
 • All choirs to prepare for a music extravaganza
 • The 500th anniversary reformation week runs 1 – 8 October 2017

AT PARISH AND INSTITUTIONAL LEVEL

1 Oct Sunday

 • Marks the beginning of the celebrations
 • A special church service needs to be conducted
 • Someone who is an authority on church history needs to be available to teach the purpose and the historical background that led to church reformation
 • A choir festival

2 Oct Monday

 • To be earmarked as a youth day.
 • Tree planting
 • Blood donation when possible
 • Visit the needy in the community in order to assist them

3 Oct Tuesday

 • A special day for men
 • Men and diakonia service
 • Pray for the sick
 • Cleaning the environment
 • A consultation for men and boys

4 Oct Wednesday

 • A special day for women
 • Women and diakonia service
 • Pray for the sick
 • Cleaning the environment
 • A consultation for women and girls

5 Oct Thursday

 • A special day for the church institutions at all levels
 • Emphasis during religious classes should be on the Reformation
 • Community service
 • Obtain information on the history of the Reformation
 • Blood donation when possible

6 Oct Friday

 • A special day for children
 • A pastor to lead a church service for children
 • A play
 • Choir or special songs

7 Oct Saturday

 • A day for all the people participate
 • Cleanliness of the environment
 • Music festival

8 Oct Sunday

 • The climax of the celebrations
 • Only one service should be held if possible
 • A mass choir should perform on that day
 • Music festival

AT NATIONAL LEVEL

 • The church has chosen Tumaini University Makumira (TUMA) to host the national celebrations to mark the 500th anniversary of the Reformation
 • A consultation will take place on 7/10/2016 during which a number of papers will be presented and discussed by representatives from all 25 dioceses of the ELCT
 • On 8/10/2017 a special church service will mark the climax of the 500th anniversary


Elizabeth Lobulu
Communication Coordinator,
Evangelical Lutheran Church in Tanzania
Box 3033, ARUSHA, Tanzania.
Phone: +255-27-250-8856/7
FAX: +255-27-254-8858
E-mail: ELobulu@elct.or.tz

Close this window

For more information contact:

Elizabeth Lobulu
Communication Desk Officer, ELCT
E-mail: ELobulu@elct.or.tz