ELCT Press Release

Date: June 29, 2017
Press release No. 001/06/2017

close window


Askofu Gaville awekwa wakfu kuongoza Dayosisi ya Iringa


Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Fredrick Shoo, akiwa na viongozi wapya
wa
Dayosisi ya Iringa kushoto ni Askofu Blaston Tuluwene Gaville na
kulia ni Mchg. Himidi John Sagga,
Msaidizi wa Askofu.

Zilikuwepo nderemo na vicheko kwa wingi Jumapili iliyopita tarehe 25 Juni, 2017 siku ambayo viongozi wa awamu ya pili katika Dayosisi ya ya Iringa ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) walipoingizwa rasmi kazini.

Katika tendo la kumweka wakfu pamoja na mambo mengine Askofu Dkt Owdenburg Moses Mdegella alimkabidhi msalaba na fimbo Askofu mteule Gaville na Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Fredrick Shoo alimwingiza kazini kuwa mmoja wapo wa maaskofu wa KKKT.

Matukio hayo yalifanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Gangilonga jirani na Ofisi Kuu ya KKKT Dayosisi ya Iringa.

Askofu Gaville aliyezaliwa 31/12/1966 kijijini Lulanzi, Wilaya ya Kilolo, Mkoani Iringa alikuwa Msaidizi wa Askofu kati ya 2006 -2016 alipochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Dayosisi ya Iringa uliofanyika Chuo Kikuu cha Iringa 6 – 7 Oktoba 2016.

Askofu Gaville alichukua nafasi iliyoachwa wazi na Askofu Dkt. Mdegella ambaye amestaafu baada ya kutumikia Dayosisi kwa miaka 30.

Masomo yake ya Shahada ya Theologia 1994 – 1998 alihitimu Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kilichopo Arusha. Mwaka 2008 – 2009 alisoma Chuo Kikuu cha Iringa na kutunukiwa Stashahada ya juu katika masuala ya Uongozi wa Kanisa na alipata Shahada ya Uzamili ya Menejimenti ya Misioni na Maendeleo ya Jamii (2011 - 2015).

Aliwahi kuwa Mchungaji kiongozi katika sharika za Tungamalenga na Kihesa na Mkuu wa Jimbo la Kusini na Jimbo la Kaskazini.


Askofu Mdegella akimkabidhi Askofu Gaville fimbo.

Mchg. Sagga aliyezaliwa 19 Juni 1971 kijijini Ilula wilaya ya Kilolo, Mkoani Iringa Mchg. Sagga ana alisoma na kuhitimu kozi mbalimbali katika Chuo Kikuu cha Iringa kama ifuatavyo: Stashahada ya Theolojia kati ya 1995-1998 na baadaye 2001-2004 Shahada ya Theolojia na alijiendeleza kimasomo Chuoni hapo na kutunukiwa Stashahada ya juu katika masuala ya Uongozi wa Kanisa na Menejimenti 2008-2009.

Pia ana Shahada ya Uzamili ya Maendeleo ya Jamii na Usimamizi wa Miradi (2012-2014) aliyopata Chuo Kikuu cha Iringa.

==================================================
Elizabeth Lobulu
Communication Coordinator,
Evangelical Lutheran Church in Tanzania
Box 3033, ARUSHA, Tanzania.
Phone: +255-27-250-8856/7
FAX: +255-27-254-8858
E-mail: ELobulu@elct.or.tz

Close this window

For more information contact:

Elizabeth Lobulu
Communication Desk Officer, ELCT
E-mail: ELobulu@elct.or.tz