ELCT Press Release

Date: March 13, 2017
Press release No. 001/03/2017

close window


KKKT kutangaza ratiba ya Juma la Matengenezo

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) litaungana na makanisa mengine duniani kuadhimisha “Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa” ambayo yatakayofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Matengenezo hayo yalianzishwa huko Ujerumani na Dkt. Martin Luther mwaka 1517 ambayo ndiyo chimbuko la kutokea kwa Kanisa la Kilutheri duniani.

Katibu Mkuu wa KKKT, Bw. Brighton Killewa, ametangaza ratiba ya “Juma la Matengenezo ya Kanisa” itakayoanza Oktoba Mosi ambapo kutakuwa na matukio mbalimbali katika Sharika zote za KKKT, vituo, Dayosisi na ngazi ya Kanisa kitaifa.

Shughuli zinazotarajiwa kufanywa na Sharika, Dayosisi na Kanisa kwa ujumla ni pamoja na kongamano, kutoa maandiko maalumu, kupanda miti, ibada, tamasha la uimbaji, kutoa huduma za kijamii kama vile kutembelea wagonjwa, usafi wa mazingira na kuchangia damu.

Upandaji wa miti ni tukio linalofanywa kama ishara na makanisa ili kuonesha kuenea na jinsi dunia nzima ilivyoguswa na matengenezo yaliyoanzia Ujerumani na kuchochea moto wa Injili ulioweza kuenea dunia nzima.

Alisema KKKT imeandaa wimbo maalumu utakaoimbwa na kwaya katika juma la matengenezo katika sharika zote na vituo vyake.

Katika ngazi ya Kanisa, kitaifa Katibu Mkuu alisema matukio mbalimbali yatafanyikia kwa siku tatu Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira ambapo watu wapatao 1,000 wanatarajiwa kuhudhuria kuwakilisha Dayosisi, maeneo ya misioni, vituo vya Kanisa.

Pia wageni mbalimbali wakiwemo washirika na wawakilishi wa makanisa dada wataalikwa.

Imetolewa na:
Ofisi ya Katibu Mkuu wa KKKT.

ELCT to release Church Reformation programme

The Evangelical Lutheran Church in Tanzania (ELCT) joins other churches all over the world in commemoration of the “500 years of Church Reformation” to take place in October 2017.

The Church Reformation that started in Germany by Martin Luther in 1517 prompted the creation of the Lutheran Church globally.

The ELCT Secretary General, Mr. Brighton Killewa, has announced the “The Reformation Week programme” to start on October 1st whereby a number of activities will take place in all ELCT parishes, institutions, dioceses and at the national level.

The activities to be done at parish, diocese and church levels include: conducting workshops; launching various pieces of literature; tree planting; church services; choir festivals and doing charity work including visiting the sick; cleaning up of the environment and blood donation.

Tree planting is a symbolic gesture taking place in all Lutheran churches showing the world wide influence and significance of the reformation that started in Gemany 500 years ago.

The ELCT has prepared a special song to be sung by all choirs in all parishes and its institutions during the Reformation Week in October.

At the national level, the church plans to have a three-day commemoration to be held at Tumaini University Makumira whereby at least 1,000 people are expeced to attend. Paricipants are from the dioceses, mission areas, and church institutions.

Various guests from partner and sister churches will also be invited.

Issued by:
ELCT Secretary General’s Office.

 

==================================================
Elizabeth Lobulu
Communication Coordinator,
Evangelical Lutheran Church in Tanzania
Box 3033, ARUSHA, Tanzania.
Phone: +255-27-250-8856/7
FAX: +255-27-254-8858
E-mail: ELobulu@elct.or.tz

Close this window

For more information contact:

Elizabeth Lobulu
Communication Desk Officer, ELCT
E-mail: ELobulu@elct.or.tz